Msimamo wa Chadema wawaibua wadau, watoa maoni tofauti

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitoa msimamo wake ikiwemo kutaka mwenyekiti wake, Tundu Lissu, kuachiwa huru bila masharti, wachambuzi wa siasa nchini wamesema ni muhimu wanasiasa kukaa meza moja kuzungumza na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.