Waziri Kombo: Kuna haja ya kuwa na viongozi wenye ujuzi wa kuzungumza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amesema kutokana na mabadiliko ya ulimwengu, kuna haja ya kuwa na viongozi wenye maarifa ya kisiasa na ujuzi wa kuzungumza, watakaosimama imara kuilinda nchi na kuitetea kwa maslahi ya Taifa.