Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Uhusiano, Deus Sangu ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha kwa viongozi wa Baraza hilo pamoja na kulitambulisha jukumu jipya la uhusiano ambalo Wizara yake imekabidhiwa kuratibu.