Walimu 606 wapatiwa mafunzo ya matumizi ya Tehama, ufundi wa vifaa

Ili kutekeleza azma ya Serikali inayolenga kuwezesha matumizi ya tehama katika kujifunzia na kufundishia kuanzia ngazi ya shule za sekondari, walimu 606 kutoka mikoa yote ya Tanzania wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya siku tano ili wawe wabobezi katika eneo hilo.