Miradi 150 ya uwekezaji kusajiliwa Zanzibar kila mwaka

Wakati mazingira na miundombinu vikiboreshwa, Zanzibar imepanga kusajili miradi isiyopungua 150 ya uwekezaji kila mwaka kupitia Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).