Shabiki aliyejichukulia umaarufu AFCON 2025

Mabadiliko ya kisasa katika michezo yamewafanya mashabiki kuachana na mbinu za jadi za kushabikia na badala yake kutumia njia mbalimbali za ubunifu kama vyombo vya muziki, michoro, mavazi ya kipekee, ngoma na mbinu nyingine za kuvutia. Katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 inayoendelea nchini Morocco, mmoja wa mashabiki waliovutia hisia za wengi viwanjani ni raia wa DR Congo, Michel Kuka Mboladinga, anayefahamika kwa jina “sanamu hai”. Kuka amepata umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wake wa kipekee ambapo husimama bila kusogea wakati wa mechi za timu yake, akiwa ameinua mkono wa kulia juu na macho yakielekezwa angani. […] The post Shabiki aliyejichukulia umaarufu AFCON 2025 appeared first on SwahiliTimes .