Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imesema itaendesha ukaguzi maalumu katika vyombo vya habari na maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kujiridhisha kuwa watu wote wanaotekeleza majukumu ya kihabari wanakidhi vigezo vilivyoainishwa kwa mujibu wa sheria. Bodi hiyo imesema imebaini kuwa kuna baadhi ya watu wasio na sifa wamerejea kutekeleza majukumu ya kihabari baada ya uchaguzi mkuu. “Bodi inatoa onyo na kuwataka watu wote wanaofanya kazi za kihabari bila kuwa na ithibati kuacha mara moja, kwani kuendelea kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 50 (2) (b) cha sheria ya huduma za habari, sura ya 229,” imesema. […] The post Bodi ya Ithibati kukagua waandishi wasio na sifa makazini appeared first on SwahiliTimes .