Marekani imetangaza kujitoa katika mashirika/taasisi 66 za kimataifa kwa maelezo kuwa hazina tija kwa maslahi ya nchi hiyo, na kwamba tathmini ya mashirika zaidi inaendelea. Uamuzi huo ambao ni utekelezaji wa sera ya “Marekani Kwanza,” utayahusu mashirika 35 yasiyo ya Umoja wa Mataifa (UN) na mashirika 31 ya umoja huo. Katika waraka huo, Trump amesema amepitia tathmini ya Waziri wa Mambo ya Nje, Marco Rubio, na kubaini kuwa ni kinyume na maslahi ya Marekani kuendelea kuwa mwanachama, kushiriki au kutoa msaada wa aina yoyote kwa mashirika yaliyotajwa. Ameelekeza wizara na taasisi zote za Serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kujiondoa […] The post Marekani yatangaza kujitoa kwenye mashirika 66 ya kimataifa appeared first on SwahiliTimes .