Katika mkutano wa hadhara unaohusisha usikilizwaji wa kero za wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, wananchi wamelalamikia kelele zinazofanywa na waendesha bodaboda, jambo linaloleta mshtuko na taharuki.