Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, ametoa wito kwa askari wa Jeshi la Polisi na watumishi wote wa umma kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na uzalendo, akisema nafasi walizonazo ni dhamana kwa jamii na si miliki binafsi.