Polisi Peter alifariki kwa upungufu wa damu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya limefafanua kuwa mtuhumiwa Peter Mwita Wanda, mkazi wa Sabasaba Tarime alifariki akipatiwa matibabu kutokana na tatizo la upungufu wa damu, baada ya kulalamika kuwa anajisikia vibaya na kuwaishwa hospitali ya Wilaya ya Tarime. Polisi wamesema mtuhumiwa huyo alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha. Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa watu wanaoandaa na kusambaza taarifa za upotoshaji mitandaoni kuziacha kwani ni kinyume cha sheria. The post Polisi Peter alifariki kwa upungufu wa damu appeared first on SwahiliTimes .