Matumaini mapya vivuko vya Kigamboni wanafunzi wakiombewa kuvushwa bure

Wakati kesho shule za msingi na sekondari nchini zikifunguliwa, Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), imeomba msaada wanafunzi kuvushwa bure kwenye vivuko vya Kampuni ya Azam vinavyovusha watu kati ya Kivukoni na Kigamboni baada ya kile chao cha 'Mv Kazi' kuharibika.