Madiwani wa Mufindi, Mafinga wanolewa ili kuongeza ufanisi wao
Madiwani katika halmashauri za Wilaya ya Mufindi na Mji Mafinga wametakiwa kutumia vizuri mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo), kuimarisha uwajibikaji, ubunifu na ufanisi wa uongozi katika utekelezaji wa majukumu yao.