Rais Samia asisitiza uhuru wa mahakama na jukumu la majaji, mahakimu kuhakikisha haki inapatikana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa uhuru wa Mahakama na jukumu la majaji na mahakimu katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote. Ameyasema hayo Januari 13, 2026, wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) uliofanyika Makao Makuu ya Mahakama, Dodoma. Aidha, Rais …