Mgomo wa wafanyabiashara wa maduka jijini Arusha uliokua umeitishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara, Rocken Adolf umesitishwa kupisha majadiliano yaliyoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude ili kupata suluhu la kudumu la mgogoro huo ambao umekua ukiibuka mara kwa mara.