Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Denis Ogesa (28) mkazi wa Nairobi nchini Kenya, kwa tuhuma za kuvunja na kuingia katika tawi la benki ya Azania iliyopo katika mji wa Namanga wilayani Longido. Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo …