Utawala wa Rais wa Ameria Donald Trump unasitisha uchakataji wa viza za uhamiaji kwa raia kutoka nchi 75, msemaji wa Wizara ya Masuala ya Kigeni alisema Jumatano, kama sehemu ya hatua kali zinazoendelea za kudhibiti uhamiaji. Hatua hiyo inafanya Kenya kuwa nchi ya pekee kutoka Afrika Mashariki na upembe wa Afrika ambayo raia wake watapata viza kuingia Amerika. Raia wa nchi za Amerika Kusini zikiwemo Brazil, Colombia na Uruguay, nchi za Balkan kama Bosnia na Albania, nchi za Asia Kusini, Pakistan na Bangladesh, pamoja na mataifa mengi barani Afrika, Mashariki ya Kati na Caribean, hawatapata viza za kuzuru Amerika Januari 21, alisema msemaji huyo. Barua wa Wizara ya Masuala ya Kigeni uliotangaza hatua hiyo na kuonekana na Reuters ulisema idara hiyo inaendesha “mapitio kamili” ya sera, kanuni na miongozo yote ili kuhakikisha “kiwango cha juu zaidi cha uchunguzi na uhakiki” kwa waombaji wote wa viza za Amerika. Barua hiyo, iliyotumwa kwa balozi za Amerika nje ya nchi, ulisema kuna viashiria kwamba raia kutoka nchi hizo wamekuwa wakitafuta msaada wa kijamii nchini Amerika. “Waombaji kutoka nchi hizi wako katika hatari kubwa ya kuwa mzigo kwa umma na kutegemea rasilmali za serikali za mitaa, majimbo na serikali ya shirikisho nchini Amerika,” ilisema barua hiyo. Hatua hiyo, iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na Fox News, haiathiri viza za wageni, ambazo zimekuwa zikivutia uangalizi mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa Amerika itaandaa Kombe la Dunia la 2026 na Olimpiki za 2028. Uamuzi huo unafuatia agizo la Novemba lililowaelekeza mabalozi wa Amerika kuhakikisha kuwa waombaji wa viza wana uwezo wa kujitegemea kifedha na hawako katika hatari ya kutegemea ruzuku za serikali wakati wa kukaa kwao Amerika, kulingana na barua ya Wizara ya Masuala ya Kigeni. “Wizara itatumia mamlaka yake ya muda mrefu kutangaza wasio na sifa wahamiaji wanaoweza kuwa mzigo kwa umma kwa Amerika na kutumia vibaya ukarimu wa wananchi wa Amerika,” alisema Tommy Pigott, Naibu Msemaji Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Kigeni. “Uchakataji wa viza za uhamiaji kutoka nchi hizi 75 utasitishwa wakati Wizara ya Masuala ya Kigeni inapopitia upya taratibu za uhamiaji ili kuzuia kuingia kwa raia wa kigeni watakaotegemea ustawi na manufaa ya umma,” aliongeza.. Orodha ya nchi zitakazoathiriwa, ni: Afghanistan, Albania, Algeria, Antigua na Barbuda, Armenia, Azerbaijan, Bahamas, Bangladesh, Barbados, Belarus, Belize, Bhutan, Bosnia, Brazil, Cambodia, Cameroon, Cape Verde, Colombia, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Cuba, Dominica, Misri, Eritrea, Ethiopia, Fiji, Gambia, Georgia, Ghana, Grenada, Guatemala, Guinea, Haiti, Iran, Iraq, Ivory Coast, Jamaica, Jordan, Kazakhstan, Kosovo, Kuwait, Kyrgyzstan, Laos, Lebanon, Liberia, Libya, North Macedonia, Moldova, Mongolia, Montenegro, Morocco, Myanmar, Nepal, Nicaragua, Nigeria, Pakistan, Jamhuri ya Congo, Urusi, Rwanda, Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent na Grenadines, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Syria, Tanzania, Thailand, Togo, Tunisia, Uganda, Uruguay, Uzbekistan na Yemen.