Zaidi ya Sh9.9 bilioni zimetumika kutekeleza miradi ya kimkakati ya ujenzi wa madaraja mawili ya Lupa na Bitimanyanga Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Mradi huo unaotekelezwa na Wakala wa Barabara (Tanroad), Mkoa wa Mbeya kwa ufadhili wa Benki ya Dunia unatajwa kuleta chachu ya kiuchumi kwa wananchi na kuchangia mapato ya Serikali.