Vijana wajitosa uhifadhi Mlima Kilimanjaro

Mradi unaoongozwa na vijana wa uhifadhi wa mazingira ujulikanao kama Guardians of the Peak – Season II umezinduliwa rasmi kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika masoko ya kimataifa ikiwemo China, pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati safi.