Jombi afokea landilodi kuhusu mtu kutembea juu ya paa usiku

MTAA WA TENA, Nairobi JOMBI mmoja katika mtaa huu alirushiana cheche za maneno na landilodi wake alipodai kuna “mtu anayetembea katika paa la nyumba kila usiku kati ya saa sita usiku na saa nane. Vurugu ilizuka pale mpangaji huyo alipomuuliza landilodi sababu ya kuweka magurudumu makuukuu juu ya paa la nyumba aliyomkodisha na kumtaka ayaondoe. “Kila siku saa sita kuna mtu anayekuja kukaa juu ya paa la nyumba yangu. Kila anapofika anakalia hizi tairi na kuanza kugongagonga paa kwa kishindo. Mimi silali. Nasumbuliwa,” jombi alimweleza landilodi. Landilodi alikanusha madai ya jamaa. Inasemekana jamaa alimwamuru landilodi kuondoa tairi hizo ama ahame hiyo nyumba yake mara moja. Kwa haraka landilodi alitafuta vijana kuondoa tairi hizo.