Matokeo ya uchaguzi Uganda kujulikana ndani ya saa 72
Zaidi ya wananchi milioni 21 nchini Uganda leo Alhamisi Januari 15, 2026 wanatarajiwa kupiga kura katika zaidi ya vituo 50,000 katika uchaguzi mkuu unaotajwa kuwa na mvutano mkali zaidi katika historia ya chaguzi za hivi karibuni nchini humo.