Familia yakabidhiwa mwili wa aliyedaiwa kujinyonga mahabusu, kuzika Jumamosi
Wakati maswali mengi yakiibuka kuhusu utata wa kifo cha Michael Rambau (18) anayedaiwa kujinyonga kwa kutumia mkanda akiwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Moshi Kati, familia imekabidhiwa mwili kwa ajili ya taratibu za maziko.