Kero ya utiririshaji majitaka Mwanza kupatiwa ufumbuzi

Kero ya utiririshaji wa maji taka na vinyesi kutoka katika maeneo ya milimani jijini Mwanza, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitishia afya na uchafuzi wa Ziwa Victoria inatarajiwa kuwa historia kufuatia kupanuliwa kwa Mradi wa Kipaumbele cha Juu cha Mwanza (Mwanza HPI).