Zaidi ya hekta 83,450 zimetengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, kwa lengo la kuzalisha jumla ya tani 250,635 za mazao ya chakula na biashara kwa msimu wa kilimo wa 2026/27, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza tija na mchango wa sekta ya kilimo katika uchumi wa halmashauri na wakulima kwa ujumla.