RC Macha akerwa na utoro kisa sare

Wanafunzi wasio na sare mkoani Simiyu hawapaswi kuzuiwa kuhudhuria masomo hasa wale wa darasa la kwanza kwa shule za msingi na kidato cha kwanza kwa shule za sekondari, kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu.