Upatikanaji dawa vituo vya afya wafikia 87%

SERIKALI imesema hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vyote vya afya nchini umefikia asilimia 87 na kwenye Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) ni zaidi ya asilimia 77. Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi amesema haya kwenye televisheni ya Azam wakati akieleza hali ya upatikanaji wa dawa na fursa za uwekezaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini. The post Upatikanaji dawa vituo vya afya wafikia 87% first appeared on HabariLeo .