Msako nyumba kwa nyumba watoto wasioripoti shuleni

DIWANI wa Kata ya Nyanguku Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Elias Ngole ametangaza kufanyika kwa operesheni maalumu kwa ajili ya kusaka watoto ambao hawajaripoti shule. Operesheni hiyo inatarajiwa kuanza Januari 19, 2026 kwa kushirikisha askari wa sungusungu watakaopita kila nyumba kusaka wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza. The post Msako nyumba kwa nyumba watoto wasioripoti shuleni first appeared on HabariLeo .