Museveni aongoza kwa asilimia 76 katika matokeo ya awali

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu yaliyotangazwa leo na tume ya uchaguzi akiwa na asilimia 76.25, huku mpinzani wake, Bobi Wine akipata asilimia 19.85. Wafuasi wa Bobi Wine wamedai kuwa kiongozi wao amezuiwa nyumbani kwake akiwa chini ya ulinzi mkali. Museveni mwenye umri wa miaka 81, ameiongoza Uganda tangu aliposhika madaraka mwaka 1986, na anatafuta ushindi mkubwa ili kuthibitisha nguvu yake ya kisiasa. Museveni aliwaambia waandishi wa habari baada ya kupiga kura yake hapo jana kuwa anatarajia kushinda kwa asilimia 80 ikiwa hakutakuwa na udanganyifu. The post Museveni aongoza kwa asilimia 76 katika matokeo ya awali appeared first on SwahiliTimes .