‘Wanafunzi Simanjiro wasizuiwe kisa sare hata wavae rubega’

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro (DC), mkoani Manyara, Fakii Lulandala amewaagiza walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari, kutowazuia kuanza masomo wanafunzi wasiokuwa na sare za shule.