Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na Bohari ya Dawa (MSD) zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kimkakati unaolenga kuelimisha na kuhabarisha jamii kuhusu masuala ya afya, sambamba na kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi, kwa wakati na zenye manufaa kwa ustawi wa wananchi.