Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limesema linawashikilia watu 8 ambao ni madereva bodaboda katika Kijiji cha Kiwambo Kata ya Kitomondo wilayani Mkuranga kwa tuhuma za kuharibu mali kwa kuvunja vioo vya mbele vya malori 16 na mabasi ya abiria mawili kwa kutumia mawe na vipande vya tofali. Polisi wamesema bodaboda hao wamefanya matukio hayo kwenye magari waliyokuwa wakikutana nayo njiani wakati wakielekea kumpumzisha mwenzao aliyefariki dunia baada ya kugongwa na gari eneo la Keko, Dar es Salaaam. Aidha, polisi wamesema pikipiki tatu walizokuwa wanatumia kama usafiri wao kutekeleza uhalifu huo zimekamatwa, na kwamba watuhumiwa hao wanashikiliwa katika kituo […] The post Bodaboda 8 mbaroni kwa kuvunja vioo vya magari 18 Rufiji appeared first on SwahiliTimes .