Auawa akidaiwa kutembea na mke wa mtu

Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Joseph Madaha, mkazi wa Kitongoji cha Kipela Magharibi, Kata ya Tumbi, Manispaa ya Tabora, amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na kisha kukatwa sikio, akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtu.