ETDCO yasaini mikataba ya umeme vitongoji 620 Katavi, Ruvuma

Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umeme (ETDCO) imesaini mikataba ya kutekeleza miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ya kusambaza umeme katika vitongoji 620 vya mikoa ya Katavi na Ruvuma, yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 95.2.