DC Maswa aweka mkazo ufaulu darasa la nne, saba

Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Dk Vicent Anney ametoa wito kwa walimu wakuu, walimu wa taaluma pamoja na wazazi na walezi kushirikiana kwa karibu ili kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi, hususan wanafunzi wa madarasa ya mitihani likiwamo la nne na la saba.