MIAKA 33 YA CHADEMA: Nafasi za uteuzi ngazi ya juu mfupa mgumu

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitimiza miaka 33 tangu kuanzishwa kwake, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa chama hicho (Bazecha), Suzan Lyimo amesema kuwanyima wanawake nafasi za juu za uteuzi ni miongoni mwa changamoto sugu inayoendelea kukikabili chama hicho.