NTSA yafuta leseni za Naekana, Monna, Greenline na Uwezo sababu ya ajali

MAMLAKA ya Kitaifa ya Uchukuzi Barabarani (NTSA) imefutilia mbali leseni za kampuni nne za uchukuzi kwa kuhusika na misururu ya ajali msimu wa sherehe Desemba mwaka jana. Kupitia taarifa, NTSA inasema ilichukua hatua hiyo baada ya kampuni hizo kushindwa kuhakikisha magari yao yanazingatia vigezo vya kiusalama. Kampuni hizo ni Monna Comfort Sacco, Greenline, Naekana Route 134 na Uwezo Coast. Madereva wao hawakuwa na maadili na walikuwa wakiyaendesha magari kwa kasi pamoja na kutozingatia sheria za trafiki. Msimamizi wa Guardina na Nanyuki nao walipewa mwanya wa siku 21 kutii maagizo yaliyowekwa na NTSA la sivyo leseni zao pia zitaondolewa.