Rais Mwinyi- SMZ yaendelea kuimarisha mazingira bora ya uwekezaji Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahakikishia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwa Serikali itaendelea kuweka vivutio na mazingira bora ya uwekezaji kwa lengo la kunufaika na miradi yao. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 20 Januari 2026, wakati wa uzinduzi wa boti mpya …