Wakati viongozi wa dunia wakikutana katika Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) huko Davos, Uswisi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa kushindwa kukabiliana na njaa kunahatarisha maisha ya watu, masoko na utulivu duniani.