Zaidi ya wafanyabiashara ndogondogo 150 wa Mtaa wa Mailimoja A, Manispaa ya Kibaha mkoani Pwani, wamepangiwa maeneo mapya ya kufanyia shughuli zao, hatua inayolenga kuwaondoa katika hatari waliyokuwa wakikabiliana nayo walipokuwa wakifanya biashara pembezoni mwa barabara ya zamani ya Morogoro.