Visiwa 65 Mwanza kupata umeme jua kwa ruzuku

Serikali inatarajia kufunga na kusambaza mifumo ya umeme wa jua katika visiwa 65 vya mkoani Mwanza kwa bei ya ruzuku, mradi utakaogharimu zaidi ya Sh4.8 bilioni.