Mirambo mwenyekiti mpya CUF akimrithi Profesa Lipumba

Hatimaye, Mirambo Yusuf amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Chama cha Wananchi (CUF) baada ya kupata kura 257 alizopigiwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa dharura wa chama hicho, uliofanyika katika Ukumbi wa Lekham, Buguruni, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumapili Februari 22, 2026.