Mvua yaua watatu Songwe, yumo mwanafunzi wa shule ya msingi

Watu watatu akiwamo mwanafunzi wa darasa la pili, wamefariki dunia kufuatia mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Songwe huku Jeshi la Polisi likiwakumbusha wananchi kuchukua tahadhari.