Katika zama hizi, ndoa nyingi haziishi tena kwa misingi ya ukweli bali kwa misingi ya maonyesho. Wanandoa wengi wamejikuta wakiishi maisha ya kuigiza, wakijenga taswira ya furaha mbele ya jamii ilhali ndani ya nyumba kuna ukimya, maumivu na migogoro isiyotatuliwa.