Wakazi Tunduru wahofia watoto kusombwa maji, walilia daraja

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Kaskazini wamemuomba Mbunge wa jimbo hilo, Ado Shaibu kuwasaidia kupata daraja katika Mto Mlingotini ili kuwanusuru watoto wao wanaosoma katika shule za msingi Nakayaya na Muungano.