Stephano Zawadi (43), mkazi wa Kitongoji cha Kambeni, Kata ya Myamba, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro amefariki dunia kwa kupigwa radi wakati alipokuwa akimfuata mkewe shambani kuzuia tumbili wasile mahindi.