RC Mara aiomba Serikali kuanza ujenzi wa Bandari ya Musoma

Serikali mkoani Mara imeishauri Wizara ya Uchukuzi kuanza mchakato wa ujenzi wa Bandari ya Musoma katika Ziwa Victoria, hatua inayotajwa kuwa chachu ya kufungua fursa za kiuchumi na kuunganisha mkoa huo na masoko ya nchi jirani za Kenya na Uganda.