MIF 2026 kujadili mikakati ya kufikia uchumi wa kati wa juu 2050

Dar es Salaam. Serikali imesema Mkutano wa Jukwaa la Wakurugenzi wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Kampuni ambazo Serikali ina hisa chache (Minority Interests Forum-MIF 2026) utakuwa jukwaa mahususi la kujadili, pamoja na mambo mengine, mikakati ya kuharakisha safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati wa juu ifikapo mwaka 2050. Mkutano huo, unaoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), utafanyika kuanzia Machi 16 hadi 18, 2026 katika Ukumbi wa PAPU, jijini Arusha, na unatarajiwa kuwakutanisha Wakurugenzi wa Bodi na Watendaji Wakuu kati ya 150 na 200 kutoka kampuni 56 ambazo Serikali inamiliki hisa chache, yaani chini ya asilimia 51. […] The post MIF 2026 kujadili mikakati ya kufikia uchumi wa kati wa juu 2050 appeared first on SwahiliTimes .