Balozi Zena: Uwezeshaji wanawake ni jambo la kimkakati, tushirikiane
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Zena Said, amesema Jukwaa la The Citizen Rising Woman ni muhimu kwa mustakabali wa taifa, hivyo amewataka wadau kuliunga mkono kwani limeonesha mwanga katika kuwainua wanawake nchini.