Rais Samia aitaka JWTZ iishi ndani ya kiapo chake

Rais Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuendelea kuishi kwa misingi ya kiapo chake, utii kwa mamlaka ya kikatiba na kuepuka vitendo vinavyoweza kuchafua heshima ya taasisi hiyo.