Jamhuri yakata rufaa kupigania ushahidi mpya kesi ya Lissu
Upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu umekimbilia Mahakama ya Rufani katika harakati za kutaka kuingiza ushahidi mpya katika kesi hiyo.